Home » Entertainment » Mad Ice asikitishwa uwepo wa Harmorapa katika muziki, ‘tunaharibu sanaa yetu’

Mad Ice asikitishwa uwepo wa Harmorapa katika muziki, ‘tunaharibu sanaa yetu’

Msanii wa muziki Bongo, Mad Ice ameelezwa kushangazwa na uwepo wa Harmorapa katika muziki na kujulikana kama msanii wakati hana uwezo huo.

Muimbaji huyo ambaye anaishi nchini Finland ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa Harmorapa anafaa katika uchekeshaji na siyo muziki na kitendo cha vyombo vya habari kuendelea kumsapoti ni kuua sanaa.

“Nimemsikia huyu Harmorapa, hapo ndipo nimekuja nimesikitika kabisa, unajua tunaharibu sanaa yetu sisi wenyewe kuna wasanii ambao wanahitaji kupewa fursa, wasanii tunajituma lakini sometime media zinatuangusha,” amesema Mad Ice.

“Nimemuana ila naona ni mtu kama ni mchekeshaji lakini ninapoona unamlinganisha na msanii kama Grace au Vanessa nitaona kuna kitu kinakusumbua kichwani,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Mad Ice amewataja Vanessa Mdee, Grace Matata na Lameck Ditto kuwa ni wasanii ambao wanatakiwa kutazamwa kama mfano kwani wanafanya muziki mzuri.

Facebook Comments

Jiunge na Mtandao wa Zotekaliblog.Com sasa!

Usipitwe na Chochote!! Jiunge na mtandao huu kupitia Facebook | Twitter | Instagram ili kupata habari na Matukio Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Zotekaliblog.Com


About Zotekali Reporter

Malik is author of Zote kali Blog, Zote kali blog is an Entertainment website based in Tanzania Local Contents and abroad for promoting and providing the latest Good Music news, Gossip and Artist news