Home » Michezo » Mbeya City yamnasa kocha Mrundi

Mbeya City yamnasa kocha Mrundi

Dar es Salaam. Wagonga nyundo wa Mbeya City wameipiga bao la kisigino Ndanda FC baada ya kumnasa kocha Ramadhan Nsanzurwimo aliyekuwa mbioni kujiunga na timu hiyo ya Mtwara.

Kocha huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ya Mbeya City ambayo ilikuwa ikisimamiwa na kocha msaidizi, Mohammed Kijuso tangu ilipoachana na Mmaalawi Kinnah Phiri.

Kabla ya kujiunga na Mbeya City, Nsazurwimo alikuwa katika hatua za mwisho kuingia mkataba na Ndanda FC, lakini mgogoro wa kiuongozi ulioibuka, ulisababisha mpango huo kuvunjika.

Taarifa iliyotolewa na afisa habari wa Mbeya City, Shah Mjanja imesema kocha huyo ataungana na timu katika kanda ya ziwa ambako ipo kwa sasa ikijiandaa na mechi zake za Ligi Kuu.

Kocha Ramadhani amewahi kuwa kocha kwa nyakati tofauti katika vilabu mbalimbali nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Malawi, Uganda, na Afrika ya Kusini, pia amewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi na kocha msaidizi na kocha mkuu wa Muda kwa timu ya taifa ya Malawi.

Facebook Comments

Jiunge na Mtandao wa Zotekaliblog.Com sasa!

Usipitwe na Chochote!! Jiunge na mtandao huu kupitia Facebook | Twitter | Instagram ili kupata habari na Matukio Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Zotekaliblog.Com


About Zotekali Reporter

Malik is author of Zote kali Blog, Zote kali blog is an Entertainment website based in Tanzania Local Contents and abroad for promoting and providing the latest Good Music news, Gossip and Artist news